MAKOSA YA KAWAIDA KWA WAONGOZAJI WENGI WA NYIMBO:
- Kutumia nyimbo nyingi katika kipindi kimoja.
- Kutumia nyimbo nyingi za zamani katika kipindi kimoja.
- Kuchagua ufunguo wa wimbo ulio juu sana.
- Kuchagua ufunguo wa wimbo ulio chini sana.
- Kuimba kwa ufunguo usio sahihi au kwa tyuni isiyo sahihi.
- Kuimba kwa sauti ya juu sana.
- Kuimba kwa sauti ya chini sana.
- Kuchagua nyimbo nyingi zinazojikita kwetu wenyewe badala ya zile zinazojikita kwa Mungu zaidi.
- Kuchagua nyimbo zenye maneno yanayochanganya/yanayogongana.
- Kuchagua nyimbo zisizokubalika kithiolojia.
- Kuchagua nyimbo zisizooana na wazo kuu la hubiri.
- Kutazamana kwa mshangao mmojawapo wa waimbaji anapokosea jukwaani na hivyo kuiathiri hadhira yote.
- Kutumia tu nyimbo zilizoandikwa na mtu binafsi kwa lengo la kibiashara.
- Kurudia sehemu moja ya wimbo mara nyingi sana.
- Kujazwa na msisimko usiotawaliwa muda wote wa kuwepo jukwaani.
- Kuimba nyimbo nyingi za haraka.
- Kuimba nyimbo nyingi za taratibu.
- Kuimba nyimbo mfululizo bila kuwa na kituo cha kufanya maombi, kusoma Maandiko, na kuishirikisha hadhira n.k.
- Mwimbishaji kuimba kwa sauti ya chini sana.
- Mwimbishaji kuimba kwa sauti nyingine badala ya sauti ya kwanza inayotumika kuimbishia.